Ujumbe wa Tanzania uliopo nchini Canada kwa ziara ya mafunzo
ukiongozwa na Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga
(aliyenyoosha mkono), ukiwa katika chumba cha kusimamia mitambo ya
kuzalisha methano (haionekani pichani) katika kiwanda cha kuzalisha
malighafi hiyo kilicho katika jimbo la Alberta nchini Canada.
Ujumbe wa Tanzania uliopo nchini Canada ukiongozwa na Naibu Waziri
Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa nne kutoka kushoto,
waliosimama), ukiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kampuni ya
kimataifa ya kuzalisha na kusafirisha methano ya nchini Canada mara
baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika kiwanda hicho. Wengine katika
picha ni Naibu Waziri, TAMISEMI, Kassim Majaliwa, (wa nne kutoka kulia,
waliosimama). Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Ummy
Mwalimu, (wa pili kutoka kulia waliosimama) pamoja na baadhi ya wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na wataalam kutoka
Wizara ya Nishati na Madini.

 


Comment