Statoil Yataja Vijana 5 Walioingia Fainali za Shindano La Mashujaa Wa Kesho

Kampuni ya Statoil Tanzania ina furaha kutangaza majina ya vijana watano waliongia fainali za shindano la biashara la mashujaa wa kesho ambalo lina dhumuni la kuhamasisha ujasiriamali kwa mikoa ya kusini mwa Tanzania yaani Mtwara na Lindi.

Akitoa taarifa hii meneja wa shindano hilo kutoka Statoil, Erick Mchome amewataja washindi hao kuwa ni Razaki Kaondo, Edward Timamu and Sifael Nkiliye (walioshiriki kama timu moja), Saleh Rashid Kisunga, Azizi Doa, na Yunus Mtopa.

Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kuwasilisha mawazo yao ya biashara ambayo baadae yalibadilishwa na kuwekwa kwenye andiko la biashara.

Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 ambao waliwasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano, na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu.

Mwazo bora yaliyopatikana kati ya 400 yalikuwa 60 na wamiliki wa mawazo hayo ambao ni zaidi ya vijana 80 kutoka Lindi na Mtwara walipewa mafunzo maalum ya kuandaa andiko la biashara ambapo yalishindanishwa tena na kupatikana vijana kumi bora waliopelekwa mbele ya majaji ambao wiki hii walichagua maandiko matano bora kati ya kumi waliyopokea.

“Vijana hawa watano watawasili jijini Dar es Salaam wiki ijayo ili kuja kutetea maandiko yao ya biashara mbele ya jopo la majaji ambao mwisho wake wataamua nani anafaa kuwa mshindi wa shindano letu,” alisema Bwana Mchome.

Mshindi wa shindano hili atatangazwa siku ya Ijumaa tarehe 15 Aprili jijini Dar es Salaam katika hafla maalum iliyoandaliwa na Statoil ili kumpongeza mshindi huyo na wenzake wanne ambao wamefanikiwa kuingia fainali. Mshindi huyo atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani 5,000 wakati washindi wanne waliobakia watapata dola 1,500 kila mmoja. Washindi wengine watano waliofanikiwa kuingia kumi bora watapata dola 1,000.

“Statoil inaamini katika kuwawezesha vijana wenye vipaji katika maeneo yote ambayo tunafanya shughuli zetu na kwa kufanya hivi tunachochea maendeleo katika maeneo hayo ambayo nasi ni sehemu yake kwani tunafanya shughuli zetu za uendelezaji wa nishati kama gesi na mafuta.,” amesema Meneja Mkazi wa Statoil Tanzania, Øystein Michelsen.

Hussein Boffu runs a consultancy helping elite entrepreneurs reach their goals through actionable business planning. Contact him via email at hussein.boffu@tanzanapetroleum.com or by calling, texting, or WhatsApp at +255(0)655376543.