Sababu 5 Kwanini Bei Ya Gesi Inapanda Wakati Inapatikana Nchini Na Hatua za Kuchukua Kuokoa Pesa Nyingi Kwa Kununua Gesi
Hivi karibuni kumeibuka mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii watu wengi wakijadili swala la kupanda bei ya gesi ya majumbani
Swala hili limepelekea kila mtanzania kuongea kile ambacho anafikiri au anavyojua. Kwa kuwa sekta ya mafuta na gesi asili bado ni changa hapa nchini watu wengi wamekuwa wakitoa taarifa ambazo sio sahihi kuhusu swala hili,
Kuna ambao wanaosema gesi ya kupikia tunayotumia sasa ni tofauti kabisa na ile inayozalishwa mtwara, kuna ambao wanaona ni bora warudi kutumia kwenye matumizi ya nishati ya mkaa na kuni ambazo ni hatari kwa mazingira na kiafya kuliko kuendelea kulipa gharama kubwa.
Kupitia makala hii utajifunza maana ya gesi tunayotumia kwa matumizi ya nyumbani, chanzo chake na vitu gani vina sababisha bei ya gesi kupanda.
Tanzania Tuna gesi Ya Kutosha hadi Kuweza Kuanza kuiuza nchi za jirani
Ukweli ni kwamba Tanzania tumebarikiwa gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trillion 57.27 . Kati ya hizo , Gesi iliyogunduliwa nchi kavu ina ukubwa wa futi za ujazo trilioni 10.17.
Gesi iliyogundulika kwenye kina kirefu cha bahari ina ukubwa wa futi za ujazo trilioni 47.08) na utafiti bado unaendelea hivyo kiwango hicho kinaweza kuongezeka muda wowote ule.
Kwa afrika masharki Tunashika namba mbili tukiongozwa na Msumbiji ambao wana gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trillion 100
Soma Hii: How-to-start-petrol-filling-station-in-Tanzania-complete-guide
Hicho ni kiwango kikubwa cha gesi ambacho si tu kinaweza kutatatua mahitaji ya nishati nchini kama vile umeme, nishati safi ya kupikia, vile vile tunaweza kuuza nishati hii kwa nchi za jirani hasa ukizingatia tunazungukwa na nchi ambazo zina mahitaji makubwa ya nishati kama Kenya Uganda ambao hawana hata lita moja ya rasilimali gesi asilia.
Swali kubwa ambalo limekuwa likiwasumbua wengi kwa nini licha ya kuwa na gesi ya ukubwa wa futi za ujazo trillion 57 bado bei ya gesi ya majumbani bado inapanda bei. Endelea kuwa nami hadi mwisho wa makala hii utajua ni kwa nini bei inapand na nini ufanye ili uepukane na adha hiyo
Chanzo cha Gesi ya Kupikia
Gesi ya kupikia ambayo unatumia hapo nyumbani au hotelini,kwa lugha ya kitaalam inaitwa LIQUEFIED PETROLEUM GAS kwa kifupi tunaita LPG
Gesi ya kupikia au LPG, huifdhiwa ikiwa katika hali ya kimiminika kwenye mitungi ya ujazo tofauti ikiwa katika mgandamizo(pressure) kubwa
Njia Mbili Za Kutengeneza Gesi Ya Majumbani
1.Kusafisha mafuta mazito (crude oil)
Yani baada ya mafuta kuvunwa kutoka kwenye visima husafisha na hapo tunaweza kupata diseli, petol, vilainishi(lubricant) na gesi ya kupikia (LPG)
Asilimi 40 tu ya gesi inayotumika majumbani hutengenezwa kwa njia hii
- Kusindika Gesi asilia
Karibu asilimia 60 ya gesi ya kupikia hutengenezwa kwa njia ya kusindika gesi asilia.
Kwa kuwa Tanzania tuna kiwango kidogo cha mafuta mazito (crude oil) maana yake hatujakuwa na uwezo bado wa kuzalisha gesi yetu ya kupikia kwa njia namba moja kama nilivoeleza hapo juu.
Lakini kwa kuwa tuna kiwango kikubwa cha gesi asilia maana yake tunaweza kuzalisha gesi yetu ya kupikia(LPG) nchini.
Lakini ili kuweza kutengeneza gesi yetu ya kupikia tunahitaji kuwa na teknologia za kisasa na pia ni gharama kubwa sana kuweza kutengeneza gesi ya kupikia kutoka kwenye gesi asilia.
Hivyo si kweli kuwa gesi tunayotumia sasa ni tofauti na ile ya Mtwara. Kwa kuwa gesi ya mtwara ni gesi asilia ambayo huitwa METHANE, na gesi ya kupikia ni (BUTANE au PROPANE) ambyo hutengenezwa kutokana na gesi hii asilia ambayo tunayo ya kutosha hapa nchini
Kwnini bei gesi Inapanda Nchini
Kama ilivyo bei ya mafuta mazito (crudi oil) gesi ya kupikia majumbani(LPG) pia hupanda au kushuka. Huu ni utaratibu wa kawaida kwenye sekta ya mafuta na gesi asilia. Yani bei ya gesi inaweza mwezi huu ikapanda baada ya mwezi mmoja ikasikia imeshuka. Kitu nachotaka uondoke nacho hapa ni kwamba, hii si mara ya kwanza na wala haitokuwa mara ya mwisho kupanda kwa gesi ya kupikia. Huenda ikapanda zaidi ya hapa au kushuka kwa kuwa ndio nature ya sekta ya mafuta na gesi
Sababu 5 Kwanini Bei ya Mafuta Inapanda Nchini
- Mabadiliko ya Bei Ya Gesi kwenye soko la kimataifa
Kama wewe ni mfatiliaji mkubwa wa masuala ya gesi na mafuta hapa nchini utagundua kuwa kiwango kikubwa cha gesi asili kama ile gesi ya pale visiwa vya songo songo, Lindi, na kule Mnazi bei Mtwara hutumika kwa kuzalishia umeme hapa nchni.
Kiwango kikubwa cha Gesi ya kupikia tunayotumia kwa sasa huagizwa kutoka mataifa ya nje. Ambapo zabuni hutangazwa na makampuni ya mafuta nchini (oil marketing companies) hugombania zabuni izo na gesi ya kupikia huingia nchnini kwa mtindo wa kuagizwa kwa pamoja yani Petroleum Bulk procurement….
Kwa kuwa gesi ya kupikia (LPG) ni bidhaa ya kimataifa hivyo kuna chombo maalum ambacho hupanga na kusimamia bei ya gesi ya kupikia dunia nzima. Hakuna nchi ambayo inaweza kwenda kinyume na prices zilizopangawa na chombo hicho hii ni Kwa sababu uwezo wetu wa kutengeneza gesi ya kupikia ni mdogo kuliko wao. Kwa sasa mamlaka ya kupanga bei ya gesi ya kupikia (LPG) dunia nzima inaitwa SAUDI ARMACO CONTRACT PRICE. Hivyo hawa wakipandisha bei ya gesi ya kupikia na Tanzania lazima bei iongezeke halikadhalika wakishusha bei.
Kwa mfano sasa bei ya gesi Kwenye soko la duni imeongeze kwa 18% na 22% hivyo imepelekea bei ya gesi ya kupikia katika soko la ndani kuongezeka kwa 8% na 11%
2.Mabadiliko ya Kifedha
Kwa kawaida bei ya gesi ya kupikia (LPG) hupangwa kufuatana na dola ya kimarekani, yani huuzwa kwa dola ya kimarekani kwa kila Tani.
Hivyo Kama dola ya kimarekani itakuwa imepanda thamani nchini kwetu, itaathiri bei ya gesi ya kupikia kwa watumiaji, mfano kwa sasa dola ya marekani imongezeka thamani nchini kwa hiyo lazima bei ya gesi ya kupikia ipande pia.
3Gharama za usafirishaji wa ge.si ya kupikia
Gesi ya majumbani (LPG)hupatikana kwenye maeneo ya uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa kuwa gesi hii hupitia maeneo mbali mbali hadi kufikia nchini kwetu, gharama za usafirishaji husababisha ongezeko la bei ya gesi ya kupikia
4.Kodi
Lakini ongezeko la kodi pia huweze kusababisha bei ya gesi ya kupikia kupanda. Kama tunavyojua lengo la wafanya biashara ni kupata faida, unapomuongezea kodi hutafuta namna ya kuongeza thamani ili apate faida. Hivyo ongezeko la kodi linaweza kusababisha kupanda kwa bei ya gesi ya kupikia
Ufumbuzi wa Kupanda kwa bei ya gesi nchini na Nini ufanye ili Ukoe Pesa nyingi kwenye Kununua gesi ya Numbani
Pamoja na kupanda kwa bei ya gesi ya kupikia bado huwezi kukwepa kutumia gesi, yani lazima ununue gesi kwa sababu zifuatazo
- Gesi ni rafiki wa mazingira kuliko nishati ya mkaa na kuni ambazo hutoa gesi chafu ya kaboni
- Kukoa muda
Pia hutumia muda mchache kwenye kupika na kukufanya kuwa na muda wa kutosha wa kufanya shughuli nyingine.
Hivyo basi suluhisho hapa ni kujua jinsi gani unaweza kuokoa pesa nyingi wakati wa kutumia gesi ya kupikia.
1.Washa jiko lako pale tu ambapo upo tayari kupika
Unandaa kila kila kitu unachohitaji kupika unakiweka tayari. Na unapowasha jiko tu unaanza kupika, hii inaokoa gesi nyingi ambayo hupotea muda ambao unakuwa umewasha jiko huku ukisubiri kuanza kupika kwa kuwa gesi hapa hufanya kazi moja tu ambayo ni kupika
2.Epuka kutumia maji mengi wakati wa kupika
Katika sufuria ya kawaida maji huchemka katika digrii 100 za centigredi. Maji yanapokuwa mengi kwenye sufuria hutumia muda mwingi kuchemka kufikia digrii za centrigredi 100 hali inayopelekea kupoteza gesi nyingi
3.Funika Sufuria ya kupikia wakati unapika
Unapokuwa unapika jitahidi kuweka kitu ambacho kitafunika sufuria ili kuzuia joto ambalo linakuwa linasambazwa kwenye maji lisiweze kupotea kama mvuke. Kadri mvuke unavyopotea ndivyo gesi zaidi inahitajika ili kufanya maji yachemke au chakula kiive
Kama unaswali lolote au maoni niandikie katika Hussein.Boffu@tanzaniapetroleum.com au piga simu 0655 37 6543
Pia weka email yako na jina lako la kwanza hapo chini na ujipatie kitabu cha bure cha kingereza kinachooelezea fursa zilizopo sekta ya mafuta na gesi Tanzania
Hussein Boffu
2015 Petroleum Geoscince Graduate