Huyu Ndiye Mtu Muhimu Sana Kwenye Sekta ya Mafuta na Gesi Duniani

images

Ni kweli ni muhimu sana huyu, kwani juhudi zake  ndo zinakufanya wewe unafurahia maisha sasa,  una uwezo wa kusafiri umbali mrefu kwa ndege au gari, unatumia internet kuwasiliana na rafiki kujifunza, una jiko la gesi, yote haya ni kwa sababu ya huyu bwana Edwin Laurentine Drake.

 Historia ya sekata ya mafuta Duniani ilizaliwa   August 27 mwaka 1859 uko Titusville Pennsylvania nchini Marekani, baada ya Edwin Laurentine Drake  ambae alifanya kazi ya ukonda kwnye gari moshi (treni) kwa miaka 8, alipochimba kisima cha kwanza cha mafuta(black gold) na kufanikiwa kuyapata katika urefu wa futi 69.5.

Kabla ya Drake Kuchimba kisima cha kwanza cha mafua katika mji wa  Titusville, Pennsylvania Nchini Marekani, watu wote ulimwnguni walikuwa wakipata mafuta katika sehemu  ambazo mafuta yalikuwa yakitiririka yenyewe toka ardhini bila kuchimbwa. Yani ilikuwa huitajiki kutumia teknolojia yoyote kuchimba mafuta, mafuta yalikuwa yanatiririka toka ardhini kama vile unavyoona chem chem za maji. Njia hii raisi ya upatikanaji wa mauta iilikuwa bado ni changamoto kwani  bado hizo chem chem zilikuwa hazizalishi kiwango kikubwa cha mafuta kukidhi mahitaji.

.wasifu wa Edwin kwa ufupi

Edwin Laurentine Drake alizaliwa tarehe 29 mwaka 1819, Katika maisha yake Edwin alifanya kazi tofauti ngumu kwa miaka 11, mwaka 1845 alijikuta akizama kwenye dimbwi la kimapenzi na kumuoa mwanadaa Philena Adam ambaye alifariki wakati alipokuwa akijifungua, Mwaka 1849 alipata kazi ya kuwa kondakta wa gari moshi(treni) ambayo aliifanya kazi hiyo kwa miaka 8. Mwaka 1957 Drake alioa tena mke mwingine Laura Dowd. Baadae Drake alilazimika kuacha kazi hiyo ya ukonda kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli.

DRAKE KUTOKA KWENYE UKONDA HADI KUAJIRIWA KWENYE KAMPUNI YA MAFUTA

Mwaka 1850 kundi la wanasheria na wakemia wa Marekani walianzisha kampuni ya kwanza ya mafuta duniani iliyoitwa “The Seneca Oil Company” Edwin alifanikiwa kupata kazi kwenye kampuni hiyo Huku kazi yake ya ukonda wa treni ikiwa kama ndio sifa iliyomfanya apate kazi hiyo kutokana na waajiri wa kampuni walikuwa wakitaka mtu ambae ataweza kusafiri vijiji vya mbali vya Pennsylvania kukusanya mafuta kwenye chem chem zilizokuwa zikitiririsha mafuta.Hivyo uzoefu wa Drake kuwa konda ilionekana atainufaisha kampuni kwani huenda akasafiri hadi vijiji eidha bure au kwa gharama nafuu.

EDWIN ANZA KUCHIMBA KISIMA WATU WAMCHEA NA KUMUITA MJINGA

Edwin alipoanza kufanya kazi na kampuni hiyo ya mafuta alifikiri namna ya kuongeza uzalishaji wa mafuta katika chem chem ambazo mafuta yalikuwa yakitiririka bila kuchimbwa (oil seeps). Katika kufikri hilo akapata wazo la kuchimba shimo ili kuweza kupata mafuta. Lakini jitihada zake ziligonga mwamba kwani alikutana na changamoto nyingi mwanzoni na kumpelekea kushindwa. Hata msaidizi wake wa uchimbaji (driller) aliyeitwa  William alianza kukata tama.Kisima(shimo) hicho ambacho Edwin alishindwa kilitwa “Drake’s folly” yani upumbavu wa Drake na baadhi ya watu ambao waliamini hataweza kufanikiwa

EDWIN ATUMIA UBUNIFU

Edwin aliamua kubadili na akaamua kutumia mabomba ya  chuma ambayo yaliweza kutoboa mwamba tabaka(sedimentary rock) aina ya shale. Ilikuwa ni august 27 1859 ambapo  alifanikiwa kuyapata mafuta (black gold) katika urefu wa futi 69. Asubuhi yake msimamizi wake alipoenda  site kukagua kazi aliona ajabu sana kuona kisima cha Drake (Drake’s well) kikitoa kiwango kikubwa cha mafuta. Inakadiriwa kisima hicho kilikuwa kina uwezo wa kuzalisha mapipa ya mafuta 20 hadi 40 kwa siku.

Matumizi ya ugunduzi wa mafuta ya Edwin Drake ulitia hamasa ubunifu wa wajasiriamali  na wagunduzi wengi duniani ambao walibuni  vitu kama magari vitakavyoweza ktumia mafuta ili kumrahisishia maisha mwanadamu.Leo hii kila anatumia kifaa au vifaa ambavyo viligunduliwa na wajasiriamali wengine baada ya Drake kugundua mafuta.Leo hii una uwezo wa kusafiri mamia na melfu ya maili za umbali kutokana na mafuta, unatumia gesi kupikia nyumbani, unatumia generata na pia mafuta na gesi kwa sasa ndo yanaendesha internet na mawasilano yote duniani.

TAFAKARI NA JIFUNZE YAFUATAYO KUTOKA KWA EDWIN DRAKE

Unadhani Ingekuwaje Drake angesikiliza maneno ya watu waliokuwa wakimuona mjinga na kumkatisha tamaa.

Unadhani  dunia ingekuwaje leo bila magari ndege,internet kama Drake angekuwa ni mtu wa kutaka majibu ya haraka na kama angekuwa mtu wa kuogopa kushindwa.

Dunia ingekuwaje kama tu baada ya kuajiriwa Drake angekuwa mtu wa kuridhika na mshahara bila kujali kufikiri ni jinsi gani anaweza kuongeza thamani kwenye kampuni, kutatua changamoto za kampuni na kuongeza uzalishaji.