Changamoto Mafunzo ya Mafuta na Gesi Vyuo Vya Tanzania

imgresLicha ya vyuo vingi nchini kuendelea kutoa mafunzo ya elimu ya gesi na  mafuta kwa vijana wa kitanzania bado kuna changamoto nyingi sana kwenye utoaji  wa mafunzo hayo.  Vyuo kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), chuo cha  madini Dodoma(MRI)   chuo cha madini Shinyanga (ESIS)  na Chuo  Kikuu cha Nelson Mandela ndio vyuo pekee Tanzania vinavyotoa mafunzo ya mafuta na gesi

Leo tutaona ni changamoto gani ambazo  elimu na mafunzo haya yanakabiliwa nazo.

Utafiti wa hali halisi ya mafunzo ya mafuta na gesi uliofanywa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Norway (NORAD) umeonyesha kwamba elimu na mafunzo ya gesi na mafuta yanayotolewa na vyuo vikuu nchini yanakabiliwa na changamoto zifuatazo: Mafunzo yamejikita sana kwenye eneo la utafutaji na uzalishaji, na kuacha maeneo mengine kama uhifadhi na usafirishaji; ukosefu wa walimu wenye ujuzi; ukosefu wa maabara na vifaa; na kuegemea kwenye nadharia zaidi kuliko vitendo.

Nini Kifanyike?

Kinachotakiwa hapa ni wanafunzi wanasoma taaluma hii ya mafuta na  gesi nchini wajiongeze wenyewe kutafuta maarifa zaidi  ili waweze kuwa bora katika taaluma hii. Wengi inapofikia hatua hii huanza kulalamika, wengine hulaumu  mfumo mzima wa nchi, huku wakijisahau wao wenyewe kuwa wanatakiwa wachukue hatua.

Kikukweli sekata hii kwa Tanzania bado ni changa sana  na inagharimu sana hadi tufikie viwango vya kimataifa. Na huende ikachujua muda sana hadi tufikie viwango vya ukweli kama Norway.

Sasa chagua moja, ujiongeze mwenyewe ili uweze kuwa bora au uendelee kulalamika huku unazidi kudidimia kwenye taaluma yako.

Hizi changamoto sijahadithiwa nazijua kwa kuwa na mimi nimesoma taaluma hizi tena hapa hapa Tanzania na nilikutana nazo.

I