TPDC waanza kutafiti gesi, mafuta Mkinga

SHIRIKA la Maendeleo ya Petrol nchini, TPDC limeanza utafiti wakijiolojia wa utafutaji mafuta na gesi katika vijiji vya Gombero mkoani Tanga.

Kutokana na hilo shirika hilo limeanza kutekeleza mradi wa uchongaji wa mashimo mafupi,visima vifupi kumi kwa ajili ya shughuli hiyo ya utafiti. Mradi huo unafanywa na kumilikiwa TPDC kwa asilimia 100.

Akizindua mradi huo Mgeologia, Amina Kagera alisema lengo kubwa la mradi huo ni kuwapa mafunzo wataalam vijana wa TPDC kwa kuwatumia wataalam wa ndani ya shirika waliobobea.

Alisema fursa  hiyo itawapa hamasa vijana kufanya tafiti mbalimbali nchini lengo likiwa ni uendelezaji wa utafutaji wa mafuta na gesi kwa faida ya watanzania wote.

“Mradi huu ulianza rasmi mwaka 2010 ukiwa na malengo ya kuwajengea uwezo wataalam wa sayansi ya utafutaji wa mafuta na gesi ambao hawakuwa na msingi wa taaluma ya kijiolojia kama wale wa fani ya jiofizikia na uhandisi”alisema Kagera

Kagera alisema mradi huo unahusisha wataalam wa kukusanya sampuli za jiolojia,jiokemikia na kuchambua sampuli, kufanya tafiti mbalimbali kuhusisha sampuli hizo na utengenezaji wa ramani za kijiolojia katika maeneo husika.

Alisema pia utaongeza thamani katika mabonde ya Tanzania ambapo shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi hufanyika.

“Mwaka 2012 hadi 2013 baada ya kazi za vitendo katika maeneo ya Kakindu na Mto kibindo karibu na bwawa la Nairobi,Gombero Mkoani Tanga wataalam waligundua uwepo mkubwa wa miamba tabaka aina ya Shalena,Silti Shale na makaa ya mawe” alisema Kagera

Naye Mkurugenzi wa Utafiti, Emma Msaky alisema malengo makuu ya mradi huo ni kuzidi kuyaanisha maeneo ya utafutaji wa mafuta na gesi ili kujua uwepo wa miamba ya uzalishaji wa nishati hizo.

Alizitaja gharama za uchorongaji wa mashimo hayo na visima hivyo vifupi ni takribani dola za Kimarekani 195,000 ambapo fedha zote hulipwa na TPDC kutoka kwenye mfuko wake wa fedha za miradi ya maendeleo.

58 replies

Comments are closed.